English instructions coming soon!

Karibu kwenye PAGE ya maelekezo ya WAX

Swahili instructions

Kabla hujaangalia maelekezo
tafadhali zingatia yafuatayo:

1. Usitoe WAX kwenye kopo kama bado hujaelewa matumizi yake na kuandaa yafuatayo: - (muhimu sana kuuliza ama kurudi kupitia maelekezo tena)

2. Andaa Powder yoyote nyeupe au Corn starch au unga lainii wa mchele (muhimu sana) utatumia kabla ya kupaka WAX kuweka ukavu wa ngozi.

3. Andaa Moistrulizer (Epuka mafuta ya nazi yanaziba vitundu) tunarecommend vaseline mgando au Alovera gel (Utatumia mwishoni ukimaliza, utakuwa unapaka, KILA SIKU BILA KUKOSA kwa matokeo mazuri (ili ngozi isireact kwa kukosa unyevu)

4. Nywele zako zisiwe ndefu ama fupi sana, zishikike na vidole sio kucha. Njia rahisi wianisha na kope za macho yako (i.e. kope za chini ziwiane na nywele za down there au ndevu, kope za juu ziwiane na kwapani) vinyeleo havina shida kwenye size.

5. Safisha eneo unalotoa nywele na maji vuguvugu (nawa/oga) then likaushe kabisa kabla hujaanza kupasha wax yako. (kadiria kiwango kidogo utaongeza baadae)

6. Sasa unaweza kupasha. Toa ya kukutosha kutumia muda huohuo usiipashe ukajatumia baadae italegea (anza kidogo kwanza then utakuwa ukiongeza) Ikitokea imebaki mwaga usiirudishie kwenye kopo. 

Option 1: Local User

Njia hii ni rahisi kama, utachemsha maji kisha yaweke kwenye chupa ya chai ili yasipoe wakati wa kupashia WAX mara kwa mara.

Option 2: Warmer User

Wax yetu ni sensitive kwa moto mkali. Jitahidi ku-set warmer yako kwenye joto dogo kabla ya kupasha bidhaa. Kumbuka kuizima mara kwa mara kuepuka wax kulainika sana.

Namna sahihi ya kukadiria joto

Hakikisha Wax inalainika kwa joto dogo,(hii sio ya kupasha na kuisubiri ipoe haitafaa) ukiikoroga ianze kuvutika kama Big-G, then pima joto na kidole kukalili texture kulingana na mazingira yako.